Uncategorized

TWIGA STARS KUANZA KAZI LEO NA MAURITANIA MASHINDANO YA UNAF

admin February 14, 2020 6:07 am



BAKARI Shime, Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Wanawake Tanzania, Twiga Stars amesema kuwa watatumia nafasi ya kualikwa kwenye mashindano ya Umoja wa Wanawake kwa nchi za Kaskazini mwa Afrika (UNAF) kiukamilifu nchini Tunisia.

Twiga Stars imealikwa kwenye mashindano hayo yanayofanyika nchini Tunisia na leo itafungua pazia kwa kuanza kucheza na timu ya Mauritania majira ya saa 7:00 mchana Uwanja wa Kram.

“Wachezaji wapo vizuri na mazoezi ambayo wameyafanya yamewaweka kwenye morali nzuri ni matumaini yetu kwamba tutapata matokeo chanya kwenye mashindano haya,” amesema.

Timu shiriki kwenye mashindano haya ni pamoja na Tunisa, Morroco, Mauritania,Algeria pamoja na Tanzania.

YANGA : PRISONS SIO WEPESI ILA TUTAPAMBANA KUPATA POINTI TATU AZAM FC YAWAITA MASHABIKI UHURU KUSHUHUDIA BURUDANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply