Uncategorized

AZAM FC BADO WAMO, LICHA YA KUCHAPWA NJE NDANI NA COASTAL UNION

admin February 16, 2020 5:22 pm


KOCHA Msaidizi wa Azam FC, Idd Cheche amesema kuwa bado wanapambana kwa ajili ya mechi zinazofuata kwenye ligi ili kuongeza kasi yao baada ya kufungwa mbele ya Coastal Union, jana, Februari 15 Uwanja wa Uhuru.

zam FC ilikubali kichapo cha mabao 2-1 wakiwa nyumbani na kuwafanya wafungwe na Coastal Union nje ndani.

Mchezo wa kwanza, Azam FC ilifungwa bao 1-0 Uwanja wa Mkwakwani na mchezo wa pili ilikubali kufungwa mabao 2-1.

“Bado tuna mechi za kucheza na wachezaji wanatambua kwamba mpira ni sehemu ya makosa, yale tuliyokosea tutayafanyia kazi ili tuendelee kufanya vizuri, mashabiki watupe sapoti,” amesema.

Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 22 na ina pointi zake 44 kibindoni.

YANGA YAIVUTIA KASI POLISI TANZANIA AUBAMEYANG AWASABABISHIA BALAA HILI NEWCASTEL IKIKUBALI KULALA NA 4G

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply