Uncategorized

AUBAMEYANG AWASABABISHIA BALAA HILI NEWCASTEL IKIKUBALI KULALA NA 4G

admin February 17, 2020 4:22 am


PIERRE-Emerick Aubameyang nahodha wa Arsenal alifungua pazia la kutupia mbele ya Newcastel United kwenye mchezo wa Ligi Kuu England wakati wakiibuka na ushindi wa mabao 4-0 alianza kufanya hivyo dakika ya 54.

Dakika mbili mbele Nicolas Pepe aliongeza msumari wa pili mbele ya Newcastel United dakika ya 57 na Mesut Ozil aliendeleza balaa dakika ya 90 kwa kupachika bao la tatu na ndani ya dakika za nyongeza msumari wa nne ulikomelewa.

Alexandre Lacazette alimalizia dakika ya 90+5 kupachika bao la nne ambalo liliwapa pointi tatu jumla Arsenal.

Kwenye msimamo ipo nafasi ya 10 ikiwa na pointi 34 huku Newcastel United ikiwa nafasi ya 13 na pointi 31 zote zimecheza jumla ya mechi 26. 

AZAM FC BADO WAMO, LICHA YA KUCHAPWA NJE NDANI NA COASTAL UNION MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply