Uncategorized

POLISI TANZANIA US KWA USO NA MTUPIAJI WAO WA ZAMANI ANAYEKIPIGA YANGA

admin February 17, 2020 2:52 pm

DITRAM Nchimbi, mshambuliaji wa Yanga kesho atakuwa kazini kumenyana na mabosi wake wa zamani kwenye mchezo wa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu Bara.

Nchimbi alisajiliwa na Yanga akitokea Polisi Tanzania alikokua akicheza kwa mkopo alipelekwa na Azam FC.

Nyota huyo mwenye mabao manne ndani ya ligi na pasi mbili za mabao alikosa mchezo wa Prisons kutokana na kuwa na kadi tatu za njano na yote aliyafunga akiwa na Polisi Tanzania.

Kwenye mchezo huo Yanga ililazimisha sare ya bila kufungana ndani ya dakika tisini,Uwanja wa Taifa.

Daktari wa timu ya Yanga,Shecky Mgazija amesema kuwa tayari adhabu ya Nchimbi imekamilka baada ya kuukosa mchezo mmoja kutokana na adhabu yake ya kadi njano tatu za njano.

POLISI TANZANIA WAIPIGA MKWARA HUU YANGA LIPULI YAACHANA NA ISHU YA SIMBA,NGUVU ZAO ZIPO HUKU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply