MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa hakustahii sare kwenye mchezo wake wa jana dhidi ya Yanga kutokana na kiwango walichoonyesha wachezaji wake ndani ya Uwanja.
Polisi Tanzania, ikiwa Uwanja wa Ushirika Moshi ilikubali sare ya kufungana 1-1 kwenye mchezo wa ligi uliokuwa na ushindani mwanzo mwisho.
Yanga ilikwenda mapumziko ikiwa inaongoza bao 1-0 lilipinduliwa kibabe na Polisi Tanzania dakika ya 61 kupitia kwa Matheo Anthon ila waamuzi walilikataa na dakika saba mbele likapichwa lingine kupitia kwa Sixtus Sabilo na kuweka mzani sawa.
Hamsini amesema:”Siwezi nikazungumza mengi kuhusu mchezo wetu dhidi ya Yanga, vijana walijituma na tulistahili ushindi matokeo tuliyopata hatukstahili,”.
Sign in
Welcome! Log into your account
Forgot your password? Get help
Password recovery
Recover your password
A password will be e-mailed to you.