Home Uncategorized KUMBE! MKWANJA NDIO ULIOMTOA NDUKI MOROCCO MBAO

KUMBE! MKWANJA NDIO ULIOMTOA NDUKI MOROCCO MBAO


UONGOZI wa Mbao FC umesema kuwa kilichomuondoa ndani ya timu hiyo aliyekuwa Kocha Mkuu Hemed Morocco ni ukosefu wa fedha unaoikabili Mbao kwa sasa.

Morocco aliomba kuondoka ndani ya Mbao akieleza kuwa sababu kubwa ni kushindwa kupata matokeo mazuri na Februari 18 uongozi wa Mbao ulithibitisha suala hilo la kuodoka kwake.

Katibu wa Mbao FC, Daniel Naila amesema :”Morocco alionba kuondoka kwenye timu yetu kutokana na kutokuwa na hela na anadai mshahara wa muda mrefu.

“Tuliomba abaki ili tujipange mambo yalikuwa magumu mwsho wa siku ameondoka. Ni kweli kwa sasa tunakabiliwa na suala la ukosefu wa fedha ndio maana tunayumba,”.

Mchezo wa kwanza ikiwa na Kocha wa Makipa, Mbao FC ilishinda mabao 21 mbele ya Singida United.

SOMA NA HII  MABOSI WA YANGA NDANI YA UZI MPYA