Uncategorized

DIDIER DROGBA APIGWA CHINI NDANI YA CAF,ETOO NDANI

admin February 21, 2020 12:52 pm


DIDIER Drogba imeelezwa kuwa amefutwa kazi yake ya ushauri wake ndani Shirikisho la soka barani Afrika CAF, katika nafasi ya kumshauri Rais wa shirikisho hilo Ahmad Ahmad.

Imeelezwa kuwa hatua hiyo imetokana na nyota huyo kushindwa kutimiza majukumu yake ya kumshauri rais huyo tangu alipoteuliwa mwezi Julai 2019.

Pia Drogba ambaye ni nahodha wa zamani wa timu ya Taifa ya Ivory Coast ameshindwa kuhudhuria au kushiriki shughuli zozote za CAF ikiwemo michuano ya AFCON mwaka jana.

Kwa sasa nafasi hiyo ya kumshauri rais Ahmad itabaki kwa mchezaji mstaafu wa Cameroon Samuel Eto’o.

HIZI HAPA DAKIKA 270 ZA MOTO KWA SIMBA KABLA YA KUINGIA MIKONONI MWA YANGA SIKU MUHIMU KWA MESSI HII HAPA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply