Uncategorized

SIMBA:TUPO TAYARI KUMALIZANA NA BIASHARA UNITED

admin February 21, 2020 10:22 am


UONGOZI wa Simba umesema kuwa maadalizi yao ya mchezo wa kesho dhidi ya Biashara United yapo sawa ni suala la wakati tu kutimiza malengo waliyojiwekea.

Simba itaikaribisha Biashara United iliyo chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 1:00 usiku.

Akizugumza na Saleh Jembe, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema kuwa hali za wachezaji zipo sawa wana imani watafanya vizuri mbele ya Biashara United.

“Wachezaji wanatambua wajibu wao hivyo suala la morali ni kazi yao kutimiza majukumu ndani ya Uwanja, mashabiki wajitokeze kwa wingi uwanjani kuipa sapoti timu yao,” amesema.

MZUNGU WA YANGA ATOA TAMKO HILI MOURINHO ABEBA MATUMAINI LIGI YA MABINGWA LICHA YA KICHAPO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply