Uncategorized

MZUNGU WA YANGA ATOA TAMKO HILI

admin February 21, 2020 9:52 am


LUC Eymael, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa wachezaji wake watapambana kupata matokeo kwenye mechi zake zinazofuata kutokana na kugundua makosa waliyoyafanya.

Yanga ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa imecheza mechi 21 na ina pointi 40, mechi yake inayofuata ni dhidi ya Coastal Union ya Tanga utakaochezwa Uwanja wa Mkwakwani, Februari 23.

“Tumekuwa na matokeo ambayo hayafurahishi ila sio mwisho wa kupambana tutafanya vizuri kwenye mechi zetu zinazofuata.

“Mashabiki watupe sapoti na kuungana nasi katika kutafuta ushindi, wachezaji wangu nimewapa majukumu yao watakuwa katika ubora,” amesema.

MTIBWA SUGAR:: VIWANJA NI TATIZO,VIBORESHWE SIMBA:TUPO TAYARI KUMALIZANA NA BIASHARA UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply