Uncategorized

YANGA YATAMBA KUPATA DAWA YA SARE, KAZI KUANZA KESHO TAIFA

admin February 25, 2020 10:14 am

JERRY Muro, aliyekuwa Ofisa Habari wa Yanga wa zamani na sasa ni mkuu wa Wilaya ya Arumeru mkoani Arusha amesema kuwa wameshapata pasword ya kuwaondolea mzimu wa sare uliokuwa unaisumbua Yanga hivyo mashabiki wajitokeze kwa wingi.

Muro amesema kuwa sare ambazo wamekuwa wakizipata zimeshapata dawa yake na kazi itaanza kesho mbele ya Gwambina FC Uwanja wa Taifa.

“Hakutakuwa na ugonjwa wa sare tena kwetu tumeshapata pasword ya hizo sare na kesho kazi inaanza rasmi mbele ya Gwambina FC.

“Napenda kuwaambia mashabiki wa Yanga wasikate tamaa kesho wajitokeze kwa wingi Uwanja wa Taifa kuona namna kikosi kitakavyoanza kazi nyumbani, ni mwendo mdundo hakuna sare tena,”.

Sare nne ilizopata Yanga ilikuwa ni kwenye mechi za Ligi Kuu Bara mbele ya Mbeya City, Tanzania Prisons, Polisi Tanzania na Coastal Union.

Yanga itamenyana na Gwambaina majira ya saa 1:00 usiku Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora Kombe la Shirikisho utakaochezwa kesho.

WILDER AMFUKUZA KOCHA ALIYETUPA TAULO ULINGONI, KOCHA MKUU AMRUKA SIMBA:TUPO TAYARI KUPAMBANA NA STAND UNITED LEO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply