Uncategorized

POGBA: SIPENDI KUONA LIVERPOOL IKITWAA UBINGWA, TULISTAHILI SISI KUUBEBA

admin February 28, 2020 4:48 am


PAUL Pogba kiungo mshambuliaji wa Manchester United amesema kuwa hapendi kuiona Liverpool ikitwaa ubingwa wa Ligi Kuu England msimu huu.

Liverpool na Manchester United ni wapinzani wakubwa jambo ambalo linawaumiza United kuiona ikitwaa ubingwa kutokana na nafasi iliyopo kwa sasa.

Kiungo huyo ambae amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu amesema kuwa ni Manchester United ilistahili kutwaa ubingwa huo ila ilikosea kwenye kuanza jambo ambalo limewaweka kwenye wakati mgumu.

“Tulikuwa na nafasi ya kutwaa ubingwa kwa kuwa tuna kikosi bora na tupo vizuri, kosa letu ilikuwa kwenye kuanza, naona Liverpool inapambana kutwaa ubingwa ila sipendi kuona ikitwaa ubingwa,” amesema.

Liverpool ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 79 huku United ikiwa nafasi ya tano na pointi zake 41 zote zimecheza mechi 27.

ISHU YA YANGA KUTWAA UBINGWA MBELE YA SIMBA IPO NAMNA HII BAADA YA KUMALIZANA NA IHEFU MACHO YA AZAM FC YAPO HUKU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply