Uncategorized

KUMEKUCHA HUKO JANGWANI, FUNGU LA KUTOSHA LAWEKWA MEZANI KUIMALIZA SIMBA

admin March 2, 2020 1:49 am

 KUELEKEA mchezo wa watani wa jadi, Yanga na Simba unaotarajiwa kuchezwa, Machi 8, Uwanja wa Taifa tayari mkwanja umewekwa mezani ili Yanga imalize mchezo huo mapema.

Imeelezwa kuwa miongoni mwa wadhamini wa Yanga, Kampuni ya GSM, imeweka mezani mamilioni ya fedha endapo Yanga itashinda mchezo huo kwa idadi yoyote ya mabao.

“Mchezo wa kwanza wachezaji waliwekewa mezani milioni mia mbili ila Ile sare ya kufungana mabao 2-2 waliambulia milioni 50 lakini safari hii mkwanja umeongezeka iwapo watashinda.

“Kinachoendelea kwa sasa ni hamasa na kuona namna gani wachezaji watapata ushindi mbele ya Simba, wameahidi kufa na kupona ili kupata mkwanja na pointi tatu,” kilieleza chanzo hicho.
MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU NAHODHA NAMUNGO ATAJA KINACHOMPA HALI YA KUJIAMINI AKIWA UWANJANI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply