Uncategorized

SIMBA YATAJA SABABU YA KIWANGO CHAO JANA KUPANDA NA KUSHUKA MBELE YA AZAM FC

admin March 5, 2020 8:05 am

FRANCIS Kahata, kiungo mshambuliji wa Simba anayefanya kazi kwa ukaribu na kiungo Jonas Mkude amesema kuwa walicheza kwa kupanda na kushuka kutokana na mpira kuwa na kanuni nyingi tofauti,

Kiungo huyo wa Simba jana alikuwa ni sehemu ya kikosi kilichoibuka na ushindi wa mabao 3-2 mbele ya Azam FC mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Taifa.

“Tulikuwa tunapanda na kushuka kutokana na aina ya mpira ambao tulikubaliana kucheza, kuna wakati tulishindwa kufanya vizuri kutokana na kutokuelewana lakini haya ni mambo ya kawaida kwenye mpira.

“Kitu kikubwa ambacho tulikuwa tunakihitaji ni pointi tatu ambazo tumezipata mashabiki watupe sapoti,”.

Jana, Machi 4, Simba ilianza kwa spidi ya chini na kuruhusu kufungwa bao la mapema dakika ya nne ambalo liliwekwa usawa na Nyoni, licha ya kushinda walionekana kucheza kwa kiwango cha kupanda na kushuka.

MPANGO MKUBWA WA MTIBWA SUGAR UPO NAMNA HII YANGA YASHUSHA PRESHA KISA SIMBA, SASA KAZI ITAKUWA NAMNA HII

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply