Uncategorized

MPANGO MKUBWA WA MTIBWA SUGAR UPO NAMNA HII

admin March 5, 2020 7:05 am
UONGOZI wa Mtibwa Sugar umesema kwa sasa mipango yao ni kuona inamaliza ligi ikiwa ndani ya 10 bora.
Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa ushindani kwenye ligi ni mkubwa na wao wanapambana kufikia malengo ambayo wamejiwekea.
“Tunajua kwamba hatujawa na msimu mzuri kwetu kutokana na kushindwa kushinda mechi nyingi hasa mwezi Februari zaidi ya saba ila haitupi mashaka tunajiamini na tunaamini malengo yetu yatakamilika kuwa ndani ya 10 bora.
“Kila mchezaji ana morali kubwa na mwalimu anawapa majukumu vijana nao wanatimiza wakati unakuja na kila mmoja atapenda,” amesema.
Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 14 ikiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 26, jana ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Namungo FC.
AZAM FC YATAJA KILICHOWAKWAMISHA TAIFA JUMLA MBELE YA SIMBA SIMBA YATAJA SABABU YA KIWANGO CHAO JANA KUPANDA NA KUSHUKA MBELE YA AZAM FC

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply