Uncategorized

AZAM FC YATAJA KILICHOWAKWAMISHA TAIFA JUMLA MBELE YA SIMBA

admin March 5, 2020 6:05 am

AGREY Moriss, nahodha wa Azam FC amesema kuwa walishindwa kupata ushindi mbele ya Simba jana Uwanja wa Taifa kutokana na makosa yao wenyewe.

Kwenye mchezo uliochezwa Machi 4, Azam ilikubali kichapo cha mabao 3-2 kutoka kwa Simba na kupeperusha pointi tatu muhimu.

“Tulianza kwa kasi na kushindwa kuzitumia nafasi ambazo tulizipata wapinzani wetu waliweza kutumia nafasi walizotengeneza wakatushinda na huu ndio mpira na haya ni matokoe, tunajipanga,” amesema. 

Azam FC imepigwa nje ndani na Simba msimu kwa jumla ya mabao 4-2, mchezo wa kwanza walifungwa bao 1-0 na mchezo wa pili walifungwa mabao 3-2.

SPIDI YA NAMUNGO INASTAHILI PONGEZI LAKINI KAMA KUNA MCHANGANYO WA SIASA ANGUKO LINAKUJA MPANGO MKUBWA WA MTIBWA SUGAR UPO NAMNA HII

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply