Home Uncategorized NAMUNGO WALIA NA UWANJA GAIRO, MOROGORO

NAMUNGO WALIA NA UWANJA GAIRO, MOROGORO

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo FC amesema kuwa kilichoiponza timu yake kusepa na pointi moja na bao moja mbele ya Mtibwa Sugar ni upana wa Uwanja wa Gairo.

Machi 4, Namungo FC ilikaribishwa na Mtibwa Sugar kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao ulikamilika kwa timu hizo kutoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa wachezaji wake wamekuwa wakipambana kutafuta matokeo ila walikwama Gairo kutokana na Uwanja wa Gairo kutokuwa rafiki kwao.

“Tunatambua kwa sasa tuna changamoto kubwa ya kutafuta matokeo kwani ligi sio mechi moja, tulishindwa kupata ushindi mbele ya Mtibwa Sugar kutokana na ugumu wa Uwanja ambao tuliutumia ulikuwa ni mpana na hatukupata nafasi ya kufanya mazoezi jioni kwa kuwa tulichelewa kufika ila kwa upande wa sehemu ya kuchezea ipo vizuri.

“Yote kwa yote bado kazi yetu ni kuendelea kujijenga na kupata matokeo kwenye mechi zetu ambazo tutacheza, mashabiki waendelee kutupa sapoti,” amesema.

Namungo FC ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 47 baada ya kucheza mechi 25.

SOMA NA HII  AJIBU AMTIA HOFU MLINDA MLANGO HUYU LIGI KUU BARA