KIKOSI cha Yanga kinachotarajiwa kuanza leo dhidi ya Simba, leo Machi 8, Uwanja wa Taifa kwa mujibu wa CHAMPIONI Jumatano na sababu zake zatajwa:-
Kipa: Farouk Shikalo, uzoefu unambeba alikuwa langoni kwenye dabi ya Januari 4, Uwanja wa Taifa, Simba 2-2 Yanga.
Beki wa Kulia: Juma Abdul inaonyesha amerejea kwenye ubora wake kwa sasa na amekuwa imara.
Beki wa Kushoto: Jafary Mohamed, kipenzi cha Kocha Mkuu, Luc Eymael.
Beki wa Kati, Lamine Moro, uwezo wa mghana huyu unaimarika kila iitwapo leo akiwa uwanjani.
Beki wa Kati: Kelvin Yondani, bado uzoefu wake unambeba licha ya kutokuwa kwenye mechi za hivi karibuni.
Kiungo Mkabaji: Papy Tshishimbi, alikuepo kwenye dabi ya Januari 4, uzoefu unambeba
Kiungo Mchezeshaji: Haruna Niyonzima, uzoefu na kasi yake vinambeba.
Winga: Balama Mapinduzi, mshuti wake bado unaishi, wengi wanatarajia kuona maajabu kwake
Mshambuliaji:- Tariq Seif, Amecheza mechi tatu za hivi karibuni akimuweka benchi, David Molinga mbele ya Coastal Union, Gwambina, Alliance
Mshambuliaji wa Kati: Ditram Nchimbi, mwili wenye nguvu na mishuti mikali, anapewa nafasi ya kuanza akiwa amefunga abao mawili ndani ya Yanga
Winga: Bernard Morrison, kiungo mshambuliaji raia wa Ghana kipenzi cha mashabiki ana nafasi ya kuanza jumla kwenye kikosi cha kwanza kutokana na uimara wake.






