Uncategorized

BAADA YA KICHAPO TAIFA KUTOKA KWA YANGA, SIMBA WATOA TAMKO

admin March 9, 2020 11:27 am

Verified

BAADA ya Simba jana kuambulia kichapo cha bao 1-0 mbele ya Yanga Uongozi umewataka mashabiki kutulia na kukubali matokeo yaliyotokea.

Ofisa Habari wa Simba Haji Manara ameandika kupitia ukurasa wake wa Instagram namna hii:-“Wanasimba wenzangu niwape salaam zangu fupi za kuwaomba kwanza tukubali tumepoteza mchezo wa jana kwa kufungwa na timu ilyocheza vizuri kuliko sie,na tukubali hilo halibadiliki kwa sasa,najua tumeumia ila hiyo ndio football tuliyoichagua kuipenda.

“Kwa tamaduni zetu lazima tucharurwe kama ambavyo tungewacharura iwapo tungeshinda,but life goes on(Maisha yanaendelea). Muhimu kujipanga kwa mchezo unaofuata keshokutwa,tusitoke ktk reli na sote tunajua ubingwa upo mikononi mwetu ,tusithubutu kumtafuta mchawi wala kulaumiana.

“Wametufunga kihalali kabisa na ni haki yao kutamba!!
But Insha’Allah tutachukua ubingwa wetu,” .

REAL MADRID YAISHIA KUPOKEA KICHAPO KUTOKA KWA REAL BETIS HIVI HAPA VIGONGO 11 VYA SIMBA MZUNGUKO WA PILI NDANI YA LIGI KUU BARA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply