Uncategorized

NAMUNGO: TUNAZITAKA POINTI TATU ZA YANGA

admin March 15, 2020 3:52 am

HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo ambaye atakuwa mwenyeji leo Uwanja wa Majaliwa mbele ya Yanga amesema anawatambua vema wapinzani wake jambo ambalo halimpi tabu.

Yanga itamenyana na Namungo kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara majira ya saa 10:00 jioni mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali.

Thiery amesema: “Ninawatambua wapinzani wangu ni timu ya aina gani, ninatambua pia mchezo utakuwa mgumu lakini tupo tayari kuzisaka pointi tatu,”.

Namungo ipo nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa imecheza mechi 27 na ina pointi 49 huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu imecheza mechi 26 ina pointi 50.

MWADUI FC WAISAMBARATISHA TANZANIA PRISONS LICHA YA KUSEPA NA POINTI TATU, POLISI TANZANIA YAKIRI KUBANWA NA NDANDA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6131

Leave a Reply