Home Uncategorized SHEVA, SUPER SUB WA SIMBA ATOA KAULI YA MATUMAINI KWA MASHABIKI

SHEVA, SUPER SUB WA SIMBA ATOA KAULI YA MATUMAINI KWA MASHABIKI


MIRAJ Athuman,”Sheva’ kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa mashabiki wasiwe na mashaka ana imani atarejea uwanjani hivi karibuni kutokana na kuwa na maendeleo mazuri.

Sheva aliumia kifundo cha mguu alipokuwa na timu ya Taifa ya Tanzania na alikitonesha kidonda hicho kwenye mchezo wa Fainali ya Kombe la Mapinduzi dhidi ya Mtibwa Sugar.

Kwenye mchezo huo uliochezwa visiwani Zanzibar, Simba ilinyooshwa bao 1-0 na kuliacha kombe likibebwa na Mtibwa Sugar.

“Naendelea vizuri kwa sasa na nina imani nitarejea uwanjani baada ya muda si mrefu kutokana na maendeleo ninayoyaona, nawashukuru mashabiki kwa sapoti na namna ambavyo wananijulia hali,” amesema.

Sheva ndani ya Simba anashikilia rekodi ya kuwa super sub, ana mabao mawili aliyofunga mbele ya Mtibwa Sugar na JKT Tanzania na alisababisha penalti kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

SOMA NA HII  YANGA YATENGA MILIONI 30 KUPATA SAINI YA MBADALA WA SARPONG