UONGOZI wa timu za Ligi Kuu Egland unatarajia kufanya kikao cha dharula siku ya Alhamsi kwa ajili ya kujadili hatma ya mwenendo wa ligi hiyo baada ya kusimamishwa mpaka Aprili 3.
Ijumaa iriripotiwa kwamba, Ligi Kuu ya England itasimama kwa muda mpaka mwezi Aprili kutokana na mlipuko wa Virusi vya Corona ambao unaendelea kwa sasa ulianza kwa kasi mwezi Januari.
Maamuzi hayo yamefikia baada ya Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta na winga wa Chelsea Callum Hudson- Odoi baada ya kukutwa wote wameathirika na Corona.
UEFA ilikaa kikao na wamiliki wa timu Jumanne ili kujua namna gani wanaweza kuvuka kikwazo cha sasa cha kusimama kwa Ligi Kuu England kwa msimu huu wa 2019/20
Baadhi ya timu zinaamini kwamba kusimama kwa ligi itakuwa ngumu kwao kutokana na malengo waliyojiwekea huku nyingine zikiamini kwamba kuna ulazima wa matokeo ya msimu mzima kufutwa ili kuanza upya kumtafuta bingwa.
Kufutwa kwa msimu itakuwa pigo kwa Liverpool ambao ni vinara wa ligi kwa sasa wakiwa wamehaha kwa muda wa miaka 30 kutafuta taji hilo na ili watwae kombe hilo wanahitaji kushinda mechi mbili tu ili kutwaa taji hilo.