Uncategorized

NYOTA WA CHELSEA AMUOMBA MSAMAHA KOCHA LAMPARD

admin March 17, 2020 8:12 am


MASON Mount nyota wa timu ya Chelsea amemuomba msamaha Kocha Mkuu wa timu hiyo Frank Lampard kwa kosa lake la kuonekana akicheza mpira akiwa na Declan Rice licha ya kukatazwa kufanywa hivyo kwenye mjumuiko wa watu.

Katazo hilo lilikuja baada ya uongozi wa Chelsea kuwaambia wachezaji wake kutochangamana na watu kutokana na agizo la Serikali kuwataka waliokaribu na wagonjwa kujitenga kwa muda wa siku 14 na jamii kwani mchezaji wao Callum Hudson-Odoi aligundulika na Virusi vya Corona wiki iliyopita.

Kiungo huyo alionekana akifurahia mtaani na rafiki yake Declan Rice kwenye kituo cha Trent Park siku ya Jumapili.

Kikosi cha kwanza cha Chelsea kilipata nafasi ya kuwa na mawasiliano ya karibu na nyota Hudson-Odoi walipokuwa kwenye kambi Cobham na ametakiwa kutoonana na wenzake kwa muda wa siku 14 baada ya kungundulika na Virusi vya Corona.

Kitendo hicho kilimfanya Kocha wa Chelsea, Frank Lampard kuzungumza na Mount kwa njia ya simu na mchezaji huyo aliomba msamaha kwa kushindwa kutimiza masharti kwani alikuwa anatambua kwamba hana maambukizi ya Corona.

UONGOZI WA YANGA WAKANUSHA ISHU YA KUMTUHUMU MKUU WA MKOA WA DAR MAISHA BANA! GHAFLA KLOPP KAGEUKA MTU WA HOFU TUPU, KADONDOSHA KARIBU KILA KITU

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply