MEDDIE Kagere mshambuliaji wa Simba ameipoteza safu ya ushambuliaji ya Yanga kwa kufunga mabao mengi kuliko washambuliaji wanne wa Yanga kwenye mechi za Ligi Kuu Bara akihusika kwenye jumla ya mabao 24 ya Simba kati ya 63 huku washambuliaji wanne wa Yanga wakihusika kwenye mabao 16 kati ya mabao 31 waliyofunga.
Kagere ametupia mabao 19 akiwa ni kinara wa utupiaji na ametoa jumla ya pasi tano za mwisho zinazokamilisha kuhusika kwenye mabao 24 huku kwa Yanga, David Molinga ni kinara wa kutupia akiwa na mabao nane akifuatiwa na Tariq Seif mwenye mabao matatu, Ditram Nchimbi amehusika kwenye mabao manne akifunga mawili na kutoa pasi za mabao mawili huku Yikpe Gnamien akifunga bao moja.
Nchimbi mwenye mabao sita alifunga mabao manne akiwa na Polisi Tanzania na alifunga mabao mawili akiwa ndani ya Yanga,jambo linalofanya safu ya Yanga ya ushambuliaji kuhusika kwenye mabao 16 wakipotezwa na idadi ya mabao ya Kagere.
Yanga safu yao ya ushambuliaji inafikisha jumla ya mabao 18 ambapo kinara wa utupiaji ni David Molinga mwenye mabao nane akifuatiwa na Ditram Nchimbi mwenye mabao sita ambapo amefunga mawili akiwa ndani ya Yanga na pasi zake zote mbili alimpa David Molinga ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar na Ruvu Shooting.
Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 71 imefunga mabao 63 huku Yanga ikiwa nafasi ya tatu ikiwa na pointi 51.