Uncategorized

DIDA ABEBA MATUMAINI YA KUTOSHA NDANI YA LIPULI FC

admin March 24, 2020 12:34 am


DEOGRATIUS Munish, ‘Dida’ mlinda mlango wa Lipuli amesema kuwa bado kikosi chao kina nafasi ya kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu Bara.


Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimamishwa kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.


Lipuli ipo nafasi ya 13 kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara imecheza mechi 29 kibindoni imekusanya pointi 33.

Dida amesema:”Wachezaji wanatambua kazi yao ni kutafuta matokeo na ninapokuwa kwenye lango huwa ninapata nafasi ya kuzungumza na mabeki wangu ili kuona namna gani tutapata matokeo chanya,”.

Lipuli imeruhusu mabao ya kufungwa 39 na imefunga mabao 35 kinara wa kutupia ni nahodha wao, Paul Nonga mwenye mabao 11 na pasi nne za mabao.
KUMBE MABEKI SIMBA WALIKAMIA MCHEZO WAO MBELE YA YANGA, MSHAMBULIAJI ALIYEWAPA TABU ASIMULIA AZAM FC YASAKA DAWA YA UBUTU WA SAFU YA USHAMBULIAJI ILIYO CHINI YA CHIRWA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply