Uncategorized

NYONI SASA KUUNGANA NA WACHEZAJI WENZAKE BAADA YA MAPUMZIKO KUISHA

admin March 24, 2020 3:34 am

BEKI mkongwe ndani ya Klabu ya Simba, Erasto Nyoni amesema kuwa anaamini kuwa atajumuika na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya pamoja baada ya mapumziko ya mwezi mmoja kukamilika.

Nyoni alipata majeraha kwenye mchezo dhidi Yanga uliopigwa Uwanja wa Taifa Machi 8 ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona kwa muda wa mwezi mmoja.

“Nina amini kwamba baada ya muda wa mwezi mmoja nina amini nitaungana na wenzangu kwenye mazoezi, kikubwa ni kuomba Mungu tuwe salama kwani hili janga ni letu sote,” amesema.

WACHEZAJI LIGI KUU BARA WAPEWA DARASA NAMNA YA KULINDA VIPAJI VYAO KOCHA NAMUNGO AWAPA PROGRAMU MAALUMU WACHEZAJI WAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply