Uncategorized

WACHEZAJI LIGI KUU BARA WAPEWA DARASA NAMNA YA KULINDA VIPAJI VYAO

admin March 24, 2020 3:04 am


NADIR Haroub, ‘Cannavaro’, Meneja wa timu ya Taifa ya Tanzania amewapa darasa wachezaji wanaokipiga Ligi Kuu Bara kuacha kubweteka kipindi hiki ambapo ligi imesimama kutokana na kuenea kwa Virusi vya Corona.

Cannavaro amewataka wachezaji kujikita kufanya mazoezi binafsi ili kulinda viwango vyao na sio kukaa kwa kuwa wamepewa mapumziko ya siku 30.


 “Wachezaji wanatakiwa wafahamu hili janga ni la dunia hivyo lazima wajiongeze kipindi hiki cha mapumziko na kufanya mazoezi binafsi ambayo yatalinda vipaji vyao.

“Jambo la msingi kwa wachezaji ni kulinda vipaji vyao endapo watatumia muda mwingi kupumzika itawaondoa kwenye reli na kuwafanya washindwe kuleta ushindani pale ligi itakapoanza,” amesema.

AZAM FC YASAKA DAWA YA UBUTU WA SAFU YA USHAMBULIAJI ILIYO CHINI YA CHIRWA NYONI SASA KUUNGANA NA WACHEZAJI WENZAKE BAADA YA MAPUMZIKO KUISHA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply