Home Uncategorized WACHEZAJI WA MTIBWA SUGAR WAPEWA KAZI YA KUWA MABALOZI

WACHEZAJI WA MTIBWA SUGAR WAPEWA KAZI YA KUWA MABALOZI


UONGOZI wa Mtibwa Sugar umewataka wachezaji wao kuwa mabalozi wazuri kipindi hiki cha mapumziko maaalumu kwa ajili ya kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

Ligi Kuu Tanzania Bara ilisimamishwa Machi 17 na Serikali pamoja na mijumuiko isiyo ya lazima kwa lengo la kupunguza maambukizi ya Virusi vya Corona ambayo kwa sasa ni janga la dunia.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar, Thobias Kifaru amesema kuwa kuna umuhimu kwa wachezaji kuwa mabalozi wazuri kwa familia pamoja na jamii kiujumla kwa kuchukua tahadhari.

“Hili ni janga la dunia hivyo wachezaji na viongozi kwa ujumla ni lazima kuchukua tahadhari ili kujilinda na Virusi hivi ambavyo wataalamu wanaeleza kuwa vinasambazwa kupitia hewa.

“Tumewapa somo wachezaji kwamba wanatakiwa kuwa mabalozi wazuri na kufuata kanuni za afya ili kuwa salama kwani afya ni muhimu katika mafanikio,” amesema.

SOMA NA HII  GSM NA YANGA WAMEFIKIA HAPA KWA SASA, UONGOZI WAFUNGUKA