Uncategorized

MASAU BWIRE: TUSISAHAU KUOMBA ILI HALI IWE SHWARI

admin April 13, 2020 9:57 am

MASAU Bwire, Ofisa Habari wa Ruvu Shooting amesema kuwa ni wakati wa kila mtanzania kuomba kwa Mungu ili janga la Corona lipite na maisha yaendelee.
Kwa sasa dunia nzima inapambana kutafuta njia ya kutoka kwenye maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo kwenye sekta ya michezo ligi nyingi zimesimamishwa kupisha maambukizi zaidi ikiwa ni pamoja na Ligi Kuu Tanzania Bara.
Akizungumza na Saleh Jembe, Bwire amesema kuwa kuna vitu vingi ambavyo dunia inakosa kwa sasa ikiwa ni pamoja na burudani ya mpira.
“Tunapita kwenye kipindi kigumu kwa sasa kila mmoja ni lazima aombe kwa Mungu wake ili tuweze kupita salama kipndi hiki kigumu na maisha yaweze kuendelea.
“Tanzania yetu na dunia inapita wakati mgumu ni lazima kila mmoja achukue tahadhari ili kuwa salama kwani hali bado haijwa shwari,” amesema Bwire.
UONGOZI WA SIMBA WAHITAJI KUONGEZA MASHINE MBILI ZA KAZI, MAJINA YAO HAYA HAPA KMC WAVUNJA KAMBI, WACHEZAJI WANAFUTILIWA KWENYE MITANDAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply