Uncategorized

MUUAJI WA SIMBA ABADILISHIWA MAZOEZI

admin April 13, 2020 10:27 am
BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amebadilishiwa program na kocha wake, Luc Eymael ambapo kwa sasa anafanya mazoezi ufukweni.

Morrison aliwafunga Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Machi 8, Uwanja wa Taifa.
Awali Morrison alikuwa akifanya mazoezi nyumbani tu katika kipindi hiki cha ligi kusimama kutokana na uwepo wa Virusi vya Corona, ambapo benchi la ufundi la Yanga liliwapa wachezaji wake wote program za kufanya wakiwa nyumbani.
Morrison amesema: “Awali baada tu ya ligi kusimama, nililazimika kununua vifaa vyangu binafsi vya mazoezi na nikawa ninafanya mazoezi ya asubuhi na jioni nikiwa nyumbani.

 “Kwa sasa hivi kocha kaniongezea mazoezi kwa kunitaka nihakikishe napata kipindi kimoja cha asubuhi au jioni cha kufanya mazoezi ufukweni,”.
VITALIS MAYANGA HAELEWI KILICHOMFANYA AWE BUTU NDANI YA KMC KOCHA COASTAL UNION AWATAKA WACHEZAJI KUCHUKUA TAHADHARI NA KULINDA VIPAJI VYAO PIA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply