Uncategorized

NDANDA YAGOMA KUSHUKA DARAJA

admin April 14, 2020 3:27 pm


VITALIS Mayanga, mshambuliaji wa Ndanda FC amesema kuwa ni ngumu kwa timu yao kushuka daraja kutokana na hesabu ambazo wanazipiga kwa sasa.

Mayanga amejiunga na Ndanda FC kwa kandarasi ya miezi mitano ambapo alirejea kwenye timu yake hiyo ya zamani akitokea KMC ambao waliamua kuachana nao kwa kile walichodai kwamba uwezo wake umeshuka.

Mayanga amesema:”Kwa sasa itakuwa ngumu kwa Ndanda kushuka daraja pale ligi itakaporejea kutokana na mikakati ambayo tumejiwekea wenyewe kwa wenyewe tukiwa ni wachezaji pamoja na uongozi.

“Malengo yetu ni kuona kwamba pale tutakaporejea kila mchezaji anatimiza wajibu wake na kujituma zaidi kwani hatukuwa kwenye nafasi mbaya, kikubwa ni kuona kwamba kwa sasa kila mmoja anachukua tahadhari na kujilinda dhidi ya Virusi vya Corona,”. 

Ndanda ipo nafasi ya 16 baada ya kucheza mechi 29 kibindoni imejikusanyia pointi 31.

MCHEKA NA NYAVU ANAYEWINDWA NA YANGA ATAJA KINACHOIMALIZA TIMU YAKE YA ZAMANI YANGA YA GSM YAJITOSA UPYA KWA MAKAMBO WA HOROYA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply