Habari za Michezo leo
Uncategorized

SIMON MSUVA ATAMANI KURUDI BONGO ILA AMEKWAMIA HAPA

admin April 16, 2020 7:01 am


SIMON Msuva nyota wa Timu ya Taifa ya Tanzania anayekipiga El Jadid ya nchini Morocco amesema kuwa kwa sasa anatamani kurudi nyumbani Tanzania ila amekwama kutokana na mipaka kufungwa.

Msuva anakipiga soka la kulipwa akiwa pamoja na mzawa mwingine Kibabage zao la Mtibwa Sugar ambaye wamekuwa wakifanya naye mazoezi nyumbani.

Wakati huu wa kujilinda na maambukizi dhidi ya Virusi vya Corona, tahadhari imekuwa ikichululiwa kwenye nchi nyingi ambao Morocco wamefunga mipaka kwa muda ili kusubiri hali iwe shwari.

Msuva amesema:”Ninaendelea salama ila nilikuwa ninapenda kurejea Bongo kuwa karibu na familia pamoja na jamaa lakini mambo yamekuwa magumu kwangu siwezi kurudi kwa sasa, sina ruhusa ya kutoka pia mipaka imefungwa.

“Kikubwa kwa sasa ni kila mmoja kuchukua tahadhari ili awe salama kwani afya ni jambo la msingi kwa kila mmoja,”.

MBELGIJI WA YANGA KULA SAHANI MOJA NA NYOTA WANNE, UONGOZI WA YANGA WATAJA MBINU INAYOTUMIKA UKIACHANA NA CHAMA, HUYU HAPA MWINGINE KUCHOMOLEWA SIMBA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply