Uncategorized

SIMBA YAWAPIGIA HESABU NYOTA HAWA WANNE, SVEN ATAJA SABABU

admin April 18, 2020 3:31 pm
SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anahitaji nyota wapya wanne ndani ya kikosi chake ambao wataongeza nguvu msimu ujao.

Sven ambaye ameiongoza Simba kwenye mechi 18 amesema anahitaji washambuliaji wawili na viungo wawili.
“Tuna kikosi kizuri hapa na nafikiria tutaendelea na kila mmoja aliyepo japokuwa tutahitaji wachezaji kadhaa wapya katika kila nafasi, kuna maeneo ya kuongeza watu kwenye kikosi hiki cha sasa,” amesema.

Miongoni mwa wachezaji wanaotajwa kuwindwa na Simba ni pamoja na Lukas Kikoti wa Namungo na Baraka Majogoro wa Polisi Tanzania ambao ni viungo huku kwa upande wa washambuliaji ni Lusajo Reliants wa Namungo na Paul Nonga wa Lipuli.
  
  
KUHUSU BILIONI 20 ZA MO NDANI YA SIMBA..A-Z YA MCHAKATO UPO HIZI MTUPIAJI POLISI TANZANIA AWAOMBA MASHABIKI KUCHUKUA TAHADHARI DHIDI YA CORONA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply