Uncategorized

MSHAMBULIAJI MWILI JUMBA, KIPENZI CHA MASHABIKI ATOA AHADI NZITO KWA MASHABIKI

admin April 20, 2020 3:29 pm


YKIPE Gnamien mshambuliaji mwili jumba anayekipiga ndani ya Yanga amesema kuwa kwa sasa anaendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona huku akijifua ili Ligi Kuu Bara ikirejea imkute kwenye ubora wake.

Nyota huyo alivunja mkataba ndani ya Klabu ya Gor Mahia ili ajiunge na Yanga kutokana na kupata dili kubwa na mabosi wa Yanga kuelewa uwezo wake.

Kwa sasa ligi imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona inatarajiwa kurejea hivi karibuni pale mambo yatakapokuwa shwari.

Gnamien amesema:”Nina amini mashabiki wa Yanga wanahitaji mambo mazuri nami pia kwa sasa ninajifua ili kuwa bora ligi ikirudi nami nitakua kwenye ubora wangu.

“Mimi nawaahidi mashabiki kufanya vizuri nao pia waendelee kutupa sapoti na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona,” .

Ndani ya Yanga ni miongoni mwa ‘super sub’ kwani bao lake la kwanza alifunga akitokea sub mbele ya Singida United Uwanja wa Namfua kwa bichwa.

HAWA JAMAA NI WAZEE WA MIPENALTI, MBABE WAO HUYU HAPA BEKI KISIKI NDANI YA INTER MILAN AIPIGIA HESABU MANCHESTER UNITED

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply