KLABU ya Barcelona imejipanga kufanya maamuzi magumu endapo tu itashindwa kufanikiwa kumpata staa wa Inter Milan, Lautaro Martinez basi itageukia kwa Real Sociedad kwa kumnasa Alexander Isak.
Barca imekuwa ikipambana kwa bidii kwa kuhakikisha inampata Martinez lakini Inter ni kama inaonekana kama haina mpango wa kumuachia staa huyo.
Klabu hiyo kwa sasa imejipanga kuona inafanikiwa kumsajili Isak ambaye anakipiga katika Klabu ya Sociedada ambako kwa msimu huu amekuwa na kiwango kizuri.
Barca mpango wake ni kumsajili straika ambaye ataongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ambayo kwa sasa wanamtegemea Messi pekee kutokana na Griezmanne kushindwa kumudu mfumo wa Barca.
Na hii ni kutokana na kwamba washambuliaji wa timu hiyo Osumane Dembele na Luis Suarez ambao wote kwa sasa ni majeruhi baada ya kufanyiwa upasuaji.
Barca imetajiwa kiasi cha euro milioni 70 kuhakikisha inafanikiwa kumsajili Isak na hii ni kutokana na kuwa na msimu bora ambao kwa sasa umepigwa stop kutokana Virusi vya Corona.
Isak alisajiliwa katika klabu hiyo akitokea Borussia Dortmund kwa kiasi cha euro 30m.