Uncategorized

KOCHA SIMBA AWATAKA AKINA LUIS WENGINE ZAIDI

admin April 21, 2020 9:29 am

SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba ameweka wazi kuwa anahitaji viungo wakali wenye uwezo mithili ya Miqussone ambao anaamini watampa matokeo ndani ya uwanja.
 Miqussone ambaye ni kiungo wa Simba kabla ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona alianza kuingia kwenye mfumo wa  Sven kutokana na kubadili matokeo akiwa ndani ya uwanja licha ya kutumia dakika chache.
Tayari Mbelgiji huyo ametoa mapendekezo yake ya aina ya wachezaji anaowataka huku akisisitiza kwamba anahitaji viungo wenye uwezo wa kunyumbulika zaidi kama ilivyo kwa Miqussone.
Akiwa amejiunga na Simba kwenye dirisha dogo la msimu huu mwezi JanuariMiqussone alicheza mechi 8 na alifunga mabao matatu na kutoa pasi moja ya bao lililofungwa na Meddie Kagere kwenye mchezo dhidi ya Bashara United na ametumia dakika 624 uwanjani.
Mechi zake hizi hapa:-JKT Tanzania (90), Mtibwa Sugar (16), Kagera Sugar (90), Biashara United (90), KMC (75) na Azam (83), Yanga (90), Singida United (90)
MEDDIE KAGERE AMJIBU KIBABE BOSSI WAKE SVEN WACHEZAJI WAPEWA SOMO HILI KULINDA VIPAJI VYAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply