Uncategorized

MANCHESTER UNITED, BARCELONA ZAKUTANA KWA MTUPIAJI HUYU FUNDI

admin April 21, 2020 7:29 am


MSHAMBULIAJI tegemeo wa Klabu ya Arsenal, Pierre Emerick Aubameyang yupo kwenye hesabu za kuwindwa na Barcelona na Manchester United.

Nyota huyo raia wa Gabon anayekipiga timu yake ya Taifa akiwa ni nahodha kwenye timu zote anazocheza ikiwa ni pamoja na Arsenal ana umri wa miaka 30.

Uwezo wake wa kutupia mabao umewavutia Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu England pamoja na mabosi wa Barcelona ambayo inashiriki La Liga.

Kabla ya Ligi Kuu England kusimamishwa kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona alitumia dakika 2,305 ndani ya uwanja na alitupia mabao 17 huku akitoa pasi moja ya bao akiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 136.

Kocha Mkuu wa Arsenal, Mikel Arteta amesema kuwa wanahitaji huduma ya nyota huyo kutokana na mchango wake mkubwa kikosini.

YANGA WACHEKELEA SAPOTI YA MDHAMINI KUMWAGA MKWANJA NYOTA POLISI TANZANIA APATA MUDA WA KUWA KARIBU NA MKE WAKE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply