Uncategorized

MASHAKA YA KOCHA MKUU LIGI KUU BARA NI KUSHUKA KWA VIWANGO VYA WACHEZAJI

admin April 22, 2020 8:35 am


ZUBER Katwila, Kocha Mkuu wa timu ya Mtibwa Sugar amesema kuwa wasiwasi wake mkubwa kwa sasa ni kushuka kwa uwezo wa wachezaji pindi ligi itakaporejea.

Katwila ni miongoni mwa wazawa ambao wanafanya kazi zake kwa umakini ndani ya Ligi Kuu Bara, anakinoa kikosi cha Mtibwa Sugar ambacho alitumia maisha yake ya soka kukipiga pia katika klabu hiyo na alitwaa taji la Ligi Kuu Bara msimu wa 1999 na 2000.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kutokana na maambukizi ya Virusi vya Corona ambavyo vinaisumbua dunia.

Katwila amesema:”Kwa wakati huu namna hali inavyokwenda mashaka yangu ni kwa wachezaji kushuka viwango vyao kwa kuwa hawapati muda wa kucheza kutokana na kuwa nyumbani.

“Mashaka yangu ni kuona kwamba wanaweza kurejea katika kasi ile ambayo waliishia ama mambo yatakuwa magumu zaidi, kikubwa wanachotakakiwa kukifanya ni kufuata program wanazopewa pamoja na kuendelea kuchukua tahadhari,”.

KOCHA KAGERA SUGAR AWATAKA WACHEZAJI WASIPUUZIE MAZOEZI KOCHA WA NAMUNGO AWATAKA WAZAWA KUTAFUTA CHANGAMOTO MPYA NJE YA BONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply