Uncategorized

MORATA: KUMKABILI DIJK NI HABARI NYINGINE

admin April 24, 2020 9:05 am

ALVARO Morata, mshambuliaji wa Klabu ya Atletico Madrid amesema kuwa kukabiliana na beki kitasa wa Liverpool, Virgil van Dijk kunahitaji akili kwani ni ngumu mithili ya kupanda mlima.

Mshambuliaji huyo amesema kuwa kupenya kwenye himaya ya beki huyo ni jambo la kujivunia kutokana na umakini wake.



Nyota huyo mwenye miaka 27 alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda mabao 4-2 dhidi ya Liverpool ambao ulikuwa ni wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.


Amewataja mabeki wengine visiki kukabiliana nao ambao ni Sergio Ramos wa Real Madrid na Giorgio Chiellini wa Juventus.


Staa huyo yupo kwa mkopo ndani ya Atletico Madrid akitokea Chelsea ambapo amecheza jumla ya mechi 38 na kutupia mabao 14.

OBREY CHIRWA ATOA NENO LA KISHUJAA AZAM FC KOCHA ALIYEPATA TABU MSIMU HUU MBELE YA YANGA LEO AMETIMIZA MIAKA KADHAA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply