Uncategorized

MPISHI WA MABAO YANGA AKUMBUKA UFUNDI WA MORRISON, AOMBA LIGI IREJEE

admin April 24, 2020 12:05 pm


JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga, amesema kuwa anaomba dua usiku na mchana janga la Virusi vya Corona lipite ili ligi irejee kutokana na kukumbuka madude ya kiungo wao, Bernard Morrison.

Abdul amesema kuwa kwa sasa wamekuwa wanyonge nyumbani kutokana na kushindwa kuendelea kucheza baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa na Serikali.

“Kuna mambo mengi ambayo nimekumbuka ndani ya ligi ikiwa na madude ya Morrison ukiachana na hayo pia namna mashabiki ambavyo walikuwa wanatupa sapoti ilikuwa ni raha.

“Muda mwingi kwa sasa ninautumia nikiwa nyumbani na mazoezi ninafanya bila uwepo wa kocha, ni balaa tupu yaani ninapenda hali irejee kama zamani maisha yaendelee,” amesema Abdul.

 Wakati ligi ikisimamishwa Abdul alihusika kwenye mabao matano kati ya 31 yaliyofungwa na Yanga ambapo alitoa pasi tano za mabao.

SIMBA SC YAKOMBA MABEKI WOTE STARS NONGA ANAWAPA TABU KWELI LIPULI FC KWA SASA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply