Home Uncategorized BALAA, KAGERE APEWA MABAO 30 LIGI KUU BARA

BALAA, KAGERE APEWA MABAO 30 LIGI KUU BARA


MSEMAJI wa klabu ya soka ya APR na mchambuzi nguli wa michezo kutoka nchini Rwanda, Clever Kazungu, amesema kuwa ana uhakika kama hali ya mambo itakuwa nzuri na Ligi Kuu Bara kurejea basi mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere atafunga mabao 30 msimu huu.
Kazungu amesema kuwa haoni uwezekano wa Kagere kukosa mabao 11 katika mechi ambazo Simba imebaki nazo.Simba imesaliwa na mechi 10 ili kukamilisha msimu ambapo itacheza jumla ya mechi 38 na Kagere kwa sasa amefunga mabao 19.
“Sina shaka na uwezo wa Kagere katika suala la kuwatungua makipa, ni mchezaji wa viwango vya juu katika eneo la ushambuliaji.
“Naamini kama hali ya mambo itakuwa nzuri na Ligi Kuu Bara ikarejea basi Kagere atafunga mabao 30 msimu huu, sioni uwezekano wa kukosa mabao 11 katika mechi ambazo klabu yake ya Simba imesaliwa nazo,” alisema Kazungu.
Kagere ambaye msimu uliopita aliibuka kinara wa upachikaji mabao baada ya kuweka kambani mabao 23, anakaribia kuivunja rekodi hiyo, mpaka sasa msimu huu amefunga mabao 19.
SOMA NA HII  MSHAMBULIAJI MPYA MBIKINAFASO AWASOTESHA YANGA UWANJA WA NDEGE