Uncategorized

ARSENAL IKIPATA OFA NONO YA AUBA INAFANYA BIASHARA

admin May 2, 2020 3:43 am


PIERRE Emerick Aubameyang, mshambuliaji wa Arsenal alijiunga na washika bunduki hao msimu wa 2018 akitokea Klabu ya Borussia Dortmund.

Nahodha huyo wa timu ya Taifa ya Gabon na Arseanl pia amekuwa na balaa uwanjani amecheza jumla ya mechi 97 kwenye mashindano yote, kacheka na nyavu mara 61 ndani ya Arsenal.

Kumekuwa na presha kubwa kwa Arsenal juu ya kubaki na nyota huyo ambaye amesema kuwa anasubiri kuona nini kitatokea kwake kuhusu Arsenal.

Inatajwa kuwa Manchester United na Barcelona zinahitaji huduma za Auba ili akaonyeshe makeke yake  ya Wakada.

Mabosi zake Arsenal inaelezwa pia hawana hiyana iwapo kutakuwa na ofa nzuri wanaweza kufanya biashara. 

KIUNGO BIASHARA UNITED ANA IMANI NA SIMBA NA YANGA KWENYE KUKUZA VIPAJI KOCHA MRUNDI AVUTIWA NA BEKI WA SIMBA MTAALAMU WA KUTENGENEZA MABAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply