Uncategorized

PELLEGRINI AZIINGIZA VITANI INTER MILAN NA JUVENTUS

admin May 3, 2020 6:13 pm


LORENZO Pellegrini nyota anayekipiga ndani ya Klabu ya Roma inayoshiriki Serie A ameziingiza vitani Inter Milan na Juventus ambazo zinaiwinda saini yake.

Kiungo huyo anayevaa jezi namba saba mgongoni kandarasi yake na Roma inadumu mpaka msimu wa 2021/22 tayari mabosi wa Roma nao wameanza mazungumzo naye ili aongeze kandarasi nyingine.

Nyota huyo mwenye miaka 23, raia wa Italia alijiunga na Roma 2017 akitokea Klabu ya Sassuolo ambapo alicheza mechi 47 tangu msimu wa 2015/17 na alitupia mabao 9.

Kwa sasa ndani ya Roma amecheza jumla ya mechi 66 na kupachika mabao sita na timu yake ipo nafasi ya tano ikiwa na pointi 45 baada ya kucheza mechi 26.

TSHABALALA YEYE MABAO YAKE NI MBELE YA WAKATA MIWA TU, SIRI YAKE HII HAPA AJIBU KUTOKUWEPO NDANI YA SIMBA MSIMU UJAO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply