Home Uncategorized HAJI MANARA APANIA KUINGIA ANGA ZA MUZIKI SASA, AWATAJA ALIOWAFUNDISHA

HAJI MANARA APANIA KUINGIA ANGA ZA MUZIKI SASA, AWATAJA ALIOWAFUNDISHA


HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema yeye amewafundisha wasanii wawili wa muziki wa Bongo fleva ambao ni Ali Kiba na Suma Lee hivyo anaamini akingia kwenye anga za uimbaji atakuwa bora zaidi.

Manara amesema amekuwa mwalimu wa Kiba na Suma Lee na ndiye alikuwa akiwateua unapofikia wakati wa kwenda kuimba linapofikia suala la kaswida.

Msemaji huyo wa Simba, amesisitiza kwamba anakaribia naye kuingia kwenye muziki huku akijigamba kwamba ana uwezo mkubwa kwa kuwa wanafunzi wake ni mahiri kwa kuimba na anaamini yeye ni mwalimu maana yake anajua zaidi.

Kiba kwa sasa anatamba na ngoma yake mpya ya Dodo ambayo inafanya vizuri kwenye chati huku Sumalee wimbo wake wa Hakunaga ulibamba na uliwahi kuwa wimbo wa taifa hivi karibuni.

SOMA NA HII  PSG YAHITAJI VIUNGO WAWILI WALIOFANYA KAZI NA POCHETTINO SPURS