Uncategorized

MTIBWA SUGAR YAZITAKA SIMBA NA YANGA ZIJIPANGE KUINGIA ANGA ZAO

admin May 15, 2020 10:11 am

UONGOZI  wa Mtibwa Sugar umesema kuwa Simba na Yanga zinapaswa zijipange kunasa saini za nyota wao kutokana na mikataba yao kuwa mirefu kwa wachezaji wao.

Miongoni mwa nyota ambao wanatajwa kuwindwa na timu hizo mbili za Kariakoo ni pamoja na Dikson Job na Kibwana Shomari ambao wote ni mabeki chipukizi.

Akizungumza na Saleh Jembe,  Ofisa Habari wa Mtibwa Sugar,  Thobias Kifaru amesema kuwa ni lazima Simba na Yanga zitazame upya sera za  kulinda vipaji vya vijana watakaowasajili ili wasipotee katika ramani.

“Timu nyingi zinatazama chuo cha mpira huku makao makuu ili wawasajili lakini wanapaswa wajipange kwani wachezaji wetu wana mikataba mirefu na pia tutaangalia na nafasi zao za kucheza kwani wengi wamekuwa wakiishia benchi kisha wanaachwa kwa sasa lazima tuangalie maslahi yao.

“Ushahidi tunao kwani hata huyu  Hassan Dilunga anayetesa kwa sasa aliwahi kusajiliwa na timu hizo akarudi nyumbani ameonekana tena hivyo ameondoka hatutapenda kuona haya yakitokea kwa hawa chipukizi,” amesema Kifaru.
HAPA NDIPO WALIPOPISHANA JEMBE NA MAREHEMU RUGE WATANZANIA WATATU WATWAA UBINGWA HUKO CONGO

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply