Uncategorized

MKE WA ICARD AKOLEZA MOTO MUMEWE KUIBUKIA ARSENAL

admin May 16, 2020 3:28 am

WANDA Nara mke wa mshambuliaji wa Paris Saint -Germain (PSG) anayecheza huko kwa mkopo akitokea Inter Milan amechochea moto wa nyota huyo kusepa ndani ya timu hiyo na kuibukia Arsenal.

Mke huyo amekoleza moto wa tetesi za mumewe kuibukia ndani ya Arsenal baada ya mtoto wao wa kiume jezi ya timu ya Arsenal ambapo inaelezwa kuwa anaweza kwenda kuwa mbadala wa Pierre Emerick Aubameyang ambaye bado hajaongeza mkataba.

Wanda ambaye ni wakala wa Icard inaelezwa kuwa kitendo cha kumvisha mwanaye jezi ya Arsenal wataalamu wa mambo wanatafsri kuwa ni dalili za mwanzo kabisa kuichochea Arsenal ifanye kweli.

Icard ametupia mabao 20 katika michezo 31 aliyocheza ndani ya PSG msimu huu na klabu hiyo pamoja na Inter Milan hazina mpango naye.

MITAMBO MIWILI YA KAZI YANGA NI BALAA, JEZI ZAO WOTE NAMBA SARE ZLATAN IBRAHIMOVIC AWINDWA NA MABOSI WA SWEDEN

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply