Uncategorized

MTUPIAJI NONGA AINGIA ANGA ZA YANGA

admin May 16, 2020 2:58 pm

PAUL Nonga, nahodha wa Klabu ya Lipuli inaelezwa kuwa yupo kwenye rada za mabosi wake wa zamani Yanga ambao wanataka kurejesha saini yake.

Nonga aliwahi kukipiga ndani ya Yanga enzi za Hans Pluijm aliomba kusepa ndani ya kikosi hicho baada ya kukosa namba kikosi cha kwanza ila kwa sasa amekuwa bora ndani ya Lipuli.

Msimu huu Nonga amevunja rekodi yake ya mabao ya msimu uliopita 2018/19 ambapo alifunga mabao matano huku msimu huu wa 2019/20 akitupia mabao 11 jambo linalowapa matumaini Yanga kuiwinda saini yake. 

 Nonga amesema kuwa ana dili nyingi mkononi ila hawezi kutaja kwa sasa atasaini wapi kwani tayari ameshawaaga mabosi zake Lipuli. “Nimeshawaaga mabosi zangu Lipuli ili watafute mbadala mwingine ila nitakapoibukia nitajua mwenyewe wakati ukifika,” amesema Nonga.

MO DEWJI FOUNDATION NA KLABU YA SIMBA WASHIRIKIANA KUGAWA BARAKOA 25,000 DAR NIYONZIMA ATUMA OMBI ZITO,KESHO NDANI YA SPOTIXTRA JUMAPILI

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply