Uncategorized

NYOTA HAWA TISA NDANI YA SIMBA MSIMU UKIMEGUKA TU WANAWEZA KUSEPA BURE KABISA

admin May 18, 2020 11:28 am


SIMBA ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zake 71 kibindoni kuna mastaa ambao maisha yao yanafika ukingoni mwishoni mwa msimu ligi ikikamilika.

Ikiwa hawatamalizana na mabosi wao Simba kwa sasa basi itakuwa njia nyeupe kwao kusepa timu nyingine bure kabisa.

Mastaa hao ni pamoja na kiungo machachari ndani ya uwanja Shiza Kichuya maarufu kama Kichuya kona, Hassani Dilunga, beki kisiki Pascal Serge Wawa raia wa Ivory Coast.

 Yusuph Mlipili beki mzawa wa kati ambaye maisha yake msimu huu yamekuwa ya tabu kikosi cha kwanza, Sharaff Eldin Shiboub kiungo raia wa Sudan.

Marcel Kaheza anayekipiga Polisi Tanzania kwa mkopo, Mohamed Rashid yeye yupo zake JKT Tanzania, Mohamed Ibrahim,’Mo Ibra’ anayekipiga Namungo pamoja na Paul Bukaba ambaye yupo zake ndani ya Namungo.

CHELSEA KUPITISHA PANGA LA KIBABE MCHAGA WA KILUVYA ALIYESHINDA JACKPOT YA SportPesa.. AKABIDHIWA UBILIONEA WAKE LEO….AFUNGUKA ALICHOFANYA…

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply