Uncategorized

KIUNGO SIMBA APATA MAJANGA MAZOEZINI

admin May 20, 2020 10:47 am

KIUNGO mshambuliaji wa Simba, raia wa DR Congo, Deo Kanda, katika mazoezi ya juzi Jumatatu yaliyofanyika katika Ufukwe wa Escape One, alijikuta akishindwa kuendelea baada ya kujitonesha kifundo cha mguu.
Kanda alijiunga na Simba mwanzoni mwa msimu huu, kwa mkopo wa mwaka mmoja, akitokea katika Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, huku akipata nafasi nzuri ndani ya klabu hiyo kiasi cha kuwa kipenzi cha mashabiki wengi nchini.

Championi Jumatano, lilibahatika kushuhudia mazoezi ya nyota huyo, katika fukwe hizo ambapo alianza kwa kukimbia na wenzake kisha kunyoosha misuli baadaye mambo yaligoma baada ya kujitonesha mguu wake na kujikuta akiishia kuwa shuhuda.
Wachezaji mbalimbali wamekuwa wakifanya mazoezi kwenye fukwe hizo ikiwa ni maandalizi ya msimu wa Ligi Kuu Tanzania Bara ambao unatarajiwa kuendelea hivi karibuni.
NYOTA PULISIC ALICHUNIWA SIKU TATU MAZIMA TAKUKURU YABAINISHA KINACHOENDELEA ISHU YA BILIONI MOJA YA MAGUFULI KWA AJILI YA AFCON

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6170

Leave a Reply