Uncategorized

TANZIA:MWALUSAKO MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA NA STARS AFARIKI

admin May 25, 2020 10:47 am


LAWRENCE Mwalusako, mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga na timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars miaka ya 1998 amefariki leo katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili alipokuwa akipewa matibabu.

Mbali ya kufanya vizuri ndani ya uwanja, aliwahi kuwa kiongozi ndani ya Yanga ambapo alikuwa Katibu Mkuu mwaka 2012 enzi za uhai wake.

Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema ni pigo kwa Taifa kwani alikuwa ni mtu wa michezo.


 “Ni pigo kwa watu wa michezo wote sio Yanga pekee, alijitoa kwa moyo katika kazi na Taifa pia, tunaendelea kutoa ushirikiano kwa familia,” amesema.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa msiba upo Kimara nyumbani kwa marehemu alipokuwa akiishi.

LIPULI YAOMBA MWENDELEZO WA SAPOTI KUTOKA KWA WADAU CORONA YATIBUA MIPANGO YA YOHANA MKOMOLA AMBAYE ANAKINUKISHA HUKO MBELE

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply