Uncategorized

MBADALA WA MROMANIA WA AZAM FC AANZA KAZI CHAMAZI

admin May 27, 2020 9:47 pm


BAHATI Vivier, Kocha Msaidizi wa Azam FC, amewasili nchini kwa ajili ya kuanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kilicho nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara na pointi zake 54.

Azam FC imeanza kufanya mazoezi yake jana Jumatano ikiwa ni maandalizi ya kumalizia mechi zake 10 zilizobaki baada ya kucheza mechi 28.


Vivier atakuwa akifanya kazi na Kocha wa Makipa, Idd Abubakar,wakisubiria kurejea nchini kwa Kocha Mkuu, Aristica Cioaba na Kocha wa Viungo, Costel Birsan, waliokwama nchini kwao, Romania.

Makocha hao wanasubiria kurejea kwa usafiri wa ndege katika anga la Ulaya mwezi ujao, kufuatia makampuni mengi ya usafiri wa anga kusimamisha shughuli zao baada ya mlipuko wa virusi vya ugonjwa wa Corona (COVID-19).

MWILI WA MWALUSAKA,MCHEZAJI WA ZAMANI WA YANGA NA TIMU YA TAIFA YA TANZANIA WAAGWA LEO MAJEMBE HAYA 22 YA KAZI SIMBA YAMERIPOTI KAMBINI, WENGINE LEO TENA

Deprecated: File Theme without comments.php is deprecated since version 3.0.0 with no alternative available. Please include a comments.php template in your theme. in /home/sokalabo/public_html/wp-includes/functions.php on line 6260

Leave a Reply